Saturday , 27th Jun , 2015

Utambulisho wa kazi mpya ya star wa michano Black Rhino, We Get It On umekwenda sambamba na hatua kubwa ya star huyo kuonesha mfano kwa vijana wenzake, kwa kuchukua hatua ya kijasiriamali kuwekeza katika sekta ya utalii hapa nchini.

Black Rhino

Black Rhino ameieleza eNewz kuwa, amechukua uamuzi huo baada ya kuona fursa kubwa iliyopo katika sekta hiyo, ikiwa na fursa nyingi kutokana na ukweli dhahiri kuwa Tanzania ni nchi ya kitalii, uchache wa nguvu kazi iliyopo sekta hiyo ikiwa ni nafasi kwa vijana kuingia na kujitengenezea vipato kuendesha maisha yao.

Black Rhino ameeleza eNewz pia kuwa, nafasi hii ya kujiajiri mwenyewe itampatia nafasi kubwa zaidi ya kufanya mambo mengine mengi, ikiwepo uhuru zaidi wa kufanya muziki wake kutokana na kutokubanwa na shughuli kama ilivyokuwa hapo zamani.

Staa huyu kabla ya kuingia katika shughuli hii mpya alikuwa ni muajiriwa wa Benki moja maarufu hapa nchini.