Monday , 28th Nov , 2016

Bank ya Barclays ambayo ina matawi yake karibuni duniani kote, inatarajia kutoa tiketi 20 kwa wanafunzi watakaofaulu mafunzo ya #ReadyToWork, kwenda kushuhudia utoaji wa tuzo kubwa Afrika Mashariki EATV AWARDS.

Bi. Helen Siria - Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka Barclays

 

Akizungumza na EATV Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka Barclays Bi. Helen Siria, amesema wanaishukuru EATV kwa kuwapa fursa hiyo ya kukutana na vijana hivyo baada ya kumaliza mafunzo ambayo wameyaandaa kwa vijana watatoa tiketi 20, ili waweze kuhudhuria usiku wa #EATVAwards.

Hivi sasa benki ya Barclays wanaendesha kampeni yao ya #ReadyToWork ambayo inawalenga wanafunzi na kutoa mafunzo ya kuweza kujiajiri, inayoendeshwa Afrika nzima.

Mtazame hapa akielezea kampeni hiyo kwa undani na jinsi ya kushiriki   https://youtu.be/MgSK5Y8SBMc

 

Tags: