Wednesday , 26th Aug , 2015

Msanii wa muziki Belle 9 anayeuwakilisha mkoa wa Morogoro amesema kuwa kama angepata uwezo mkubwa kifedha na ushirikiano na wadau wa muziki basi angefanya ziara mbalimbali za muziki katika wilaya na mitaa ili kupata sapoti zao.

staa wa miondoko ya bongofleva Belle 9

Belle 9 ambaye hivi sasa yupo katika kazi pia ya kufufua vipaji vya wasanii wachanga, amejiandaa kushoot video ya wimbo wake alioupa jina 'Shauri Zao' ameongea na eNewz kuwa hivi sasa anaendelea kuwapa sapoti wasanii chipukizi mkoani Morogoro na ndoto yake kubwa ni kufanya ziara ya muziki mkoani humo.