Saturday , 5th Sep , 2015

Staa wa muziki kutoka kanda ya kaskazini, Bee Man anayefanya shughuli zake chini ya lebo ya Lovechild iliyopo Nairobi nchini Kenya, amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi siku ya jana baada ya kuugua ghafla.

Bee Man

eNewz tumeongea na Bee Man akiwa safarini kuelekea msibani siku ya leo, ambapo ametoa taarifa hizo rasmi kwa mashabiki wake kama anavyoeleza mwenyewe hapa.

ENewz tunamtakia faraja Bee Man katika kipindi hiki kigumu na yeyote yule anayeguswa na msiba huo kwa namna moja ama nyingine, na tunaitakia roho ya marehemu mapumziko mahala pema peponi Aamin.

Tags: