Thursday , 2nd Jul , 2015

Star wa nchini Uganda, Bebe Cool ameendelea kushikilia msimamo kuwa, kwa upande wake staa wa muziki Eddy Kenzo ni msanii anayechipukia, licha ya mafanikio ya kitaifa na kimataifa ambayo Kenzo ameendelea kuyapata kupitia kazi zake.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Bebe Cool akiwa na wasanii mbalimbali stejini

Msimamo wa Bebe Cool unaenda sambamba na imani kuwa, Wimbo maarufu wa Kenzo, Sitya Loss umempatia umaarufu zaidi nje ya nchi na kumuwezesha kupata tuzo kutokana na kunakshiwa na dansi ya kuvutia kutoka kwa kundi maarufu la kudansi la watoto la Ghetto Kids huko Uganda.

Sambamba na maneno hayo, star huyo amejitapa kuwa mafanikio yake hadi kufika ngazi za kimataifa hayakumtegemea mtu yoyote yule, akihitaji tu sapoti ya mashabiki wake kumuwezesha kushinda tuzo za kituo maarufu cha Televisheni duniani kwa upande wa Afrika, kwa kumpigia kura kwa wingi.