Monday , 27th Jul , 2015

Mratibu wa Dance100% 2015 kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Kwerugira Maregesi ameelezea kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza siku ya jana katika mashindano hayo makubwa jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Dance100% 2015 kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Kwerugira Maregesi

Maregesi ameyataka makundi hususan yale yatakayoshiriki usaili utakaofuata kuwekeza nguvu katika mitindo ya kudansi zaidi na si sarakasi, ikiwa ni moja ya kigezo kikubwa ambacho majaji hutumia kutoa alama.

Kujionea kwa urefu yote yaliyojiri pale TCC Chang'ombe, kile majaji walichokisema kuhusiana na usaili wa kwanza, tazama show kali ya Dance100% 2015, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12:30 jioni, hapa EATV pekee.