
Barnaba ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kuwa anaamini anauwezo mzuri wa kutengeneza nyimbo nzuri bila video, ingawa video nazo zina umuhimu wake.
"I am the best mimi sitegemeagi video, audio zangu zenyewe zinafanyaga vizuri na zina play part kubwa, of course video lazima iwe mzuri kutokana na rotation na teknolojia ilivyobadilika, siwezi sema tu i am proffesional wakati wenzangu wanaenda na utandawazi, lazima nifanye video nzuri, kiukweli na ushindani upo lakini video yangu ntaifanya pale kwenye kiwango kinachostahili na ninajiweza, nikiona nimeshindwa basi ndio changamoto", alisema Barnaba.
Pamoja na wimbo huo Barnaba pia anakusudia kutoa video ya wimbo wa Marry you aliomshirikisha msanii kutoka hapa nyumbani Mr. Blue, ambayo wengi walidhani kuwa ameipotezea.
"Mpango upo wa kufanya Mary you na ninafanya pia nje ya nchi, kwa hiyo kuna namna ambayo nimeamua kufanya muziki wangu kwenye biashara", alisema Barnaba.
Barnaba amesema kwa sasa ana management yake mwenyewe ambayo hivi karibuni ataiweka wazi.