Thursday , 15th Sep , 2016

Msanii Baraka The Prince amejitabiria kuchukua tuzo kwenye EATV AWARDS, kutokana na ubora wa kazi zake na mashabiki wake.

Baraka

Akizungumza na East Africa Radio, Baraka The Prince amesema anazisubiri kwa hamu kubwa tuzo hizo, kwani anaamini atakuwa mmoja wa washindi wa tuzo hizo kwani ana vigezo vya kushiriki.

"Nazingoja kwa hamu sana na naamini ninazo kibao tu, na kwa sababu nina fanbase nzuri na mashabiki kibao, halafu mimi mtu hata kama sio shabiki wangu ukisikiliza muziki wangu utaku-convince tu ku-vote, kwa hiyo kwa nguvu za Mungu nategemea, kama sio mbili tatu hata moja itanitosha", alisema Baraka The Prince.

Baraka ambaye wiki hii ameachia kazi yake mpya akiwa na msanii Alikiba, amesema tuzo hizo ni jambo jema kwa wasanii, hivyo ana imani kubwa ataibuka mshindi.

Tags: