Monday , 21st Jul , 2014

Aliyewahi kutwaa tuzo maarufu za muziki za gospel nchini Kenya katika kipengele cha msanii bora wa kiume wa mwaka huu Bahati, anatarajia kutoa albamu yake mpya mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

mwimbaji muziki wa injili Kenya Bahati

Nyota huyo anayetamba na kibao maarufu kilichobatizwa jina 'Barua' ameelezea kuwa albamu yake hiyo mpya ameibatiza jina 'Barua Za Bahati'.

Bahati ameongezea kuwa katika kuwakusanya mashabiki wake anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu hiyo bila ya kiingilio chochote zaidi ya kuuza nakala za albamu yake mlangoni.