Monday , 20th Jul , 2015

Star wa muziki wa miondoko ya Bongofleva Baby Madaha hivi sasa ameamua kutumia sanaa yake ya uigizaji katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanarudisha nyuma maendeleo hasa kwa vijana ambao ni taifa la kesho.

msanii wa muziki na muigizaji filamu nchini Tanzania Baby Madaha

Baby Madaha ameongea na eNewz kuwa hivi sasa anamiliki kampuni yake binafsi akielezea kuwa filamu hiyo mpya ambayo ipo mbioni kukamilika iliyobatizwa jina la 'Saint And Ghost' imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwemo Mzee Chilo, Bella fasta, Bi Moza na wengineo wengi.

Madaha afunguka zaidi kuhusiana na filamu hiyo mpya.