Sunday , 20th Dec , 2015

Baada ya uzushi kusambaa dhidi yake kuwa muziki wake ulizorota kutokana na kushikiliwa akili na mwanaume, Nyota wa muziki Baby J aweka wazi kwamba hakuna mwanaume aliyemzuia kuendelea na muziki wake licha ya mahusiano yake ya awali kuingia dosari.

Nyota wa muziki Baby J kutoka kisiwani Zanzibar

Baby J nyota anayetokea kisiwani Zanzibar ameongea na enewz kuwa amepitia changamoto nyingi baada ya kuachana na mumewe ila mpaka sasa ameamua kusiama imara zaidi na kuelekeza nguvu zake katika muziki na sio tena mahusiano yeyote ya kimapenzi.

Aidha Baby J ambaye ni mwanamuziki amesema kuwa akiwa kama msanii ameweka wazi role models wake ambao wanampa hamasa sana katika sekta ya burudani nchini akiwafagilia waigizaji Lulu Michael, Wema Sepetu , huku hakuacha kumpa sifa msanii wa muziki kutoka Kenya Amani na Rihanna.