Saturday , 1st Aug , 2015

Msanii wa kimataifa wa Muziki kutoka nchini Tanzania Ambwene Yesaya A.Y amesema kuwa Wasanii wengi wa Tanzania wanashindwa kufika anga za kimataifa kutokana na kutoka na network ya kufamiana na watu vya kutosha.

AY

AY akiongea na Enews amesema Network na Kujuana na Watu mbalimbali ndio inayoweza kumsaidia msanii kupiga hatua katika kazi yake na kufanya vizuri katika Game.

A.Y amesema kuwa wasanii wengi bila kuwa chini ya Uongozi hawawezi kufanya chochote ndio maana akaamua kujitolewa kuwasimamia wale ambao anaamini wanaweza kufika mbali wakiwa chini ya Usimamizi.