Monday , 25th May , 2015

Asilimia 70 ya waafrika, wakiaminika kuwa chini ya umri wa miaka 35 wapo katika matarajio ya kufaidika na uwekezaji atakaoufanya staa wa muziki Akon kutoka Marekani, kufikisha umeme kwa zaidi ya waafrika milioni 600.

msanii wa muziki wa nchini Senegal Akon

Kwa sasa msanii huyo mwenye asili ya Senegal amejipanga kwa ajili ya kujenga chuo huko Bamako, ambapo kitakuwa kikifundisha wataalam katika sekta hiyo ya umeme kwa ajili ya kuendeleza mradi huo kupitia mpango wake wa Akon Lights Africa.

Huu ni uwekezaji mkubwa kabisa ambao staa huyo wa muziki ameuanza kwa lengo la kutoa mchango wake kuendeleza bara hili ambalo ndilo asili yake, kutokana na mafanikio yake ya kimuziki.