Tuesday , 31st May , 2016

Msanii wa Filamu Bongo Rose Ndauka amefunguka dhidi ya wanaodai ameshindwa kufanya mziki baada ya muda mrefu kupita tangu atangaza kuwa ameanzisha Lebo ya muziki na anawasanii anawasimamia lakini hadi leo kimya.

Msanii wa Filamu bongo Rose Ndauka

Akizungumza na eNewz Rose alisema kuwa yeye hajashindwa kufanya hivyo kwa kuwa tayari anawasanii ambao wameshawasajili wakiwa na nyimbo zao tayari na kudai kuwa yeye peke yake hawezi kwakuwa hafahamu kitu kuhusu muziki lakini kwa kusaidiana na wataalamu ambao yupo nao watakamilisha tu hivi karibuni

Aidha, Rose aliweza kutoa maoni yake kuhusiana na kauli iliyokuwa imetolewa na nguli wa filamu nchini Bibi Hindu dhidi ya wasanii wa kike wa Bongo movie kuhusu uvaaji wao wa nusu uchi mpaka kufikia filamu kushindwa kuangaliwa na watoto wakiwa na wazazi wao,

"Hakuna shida mtu kuvaa kimini kama mtu ana mguu unamruhusu kuvaa hivyo inategemea na uhusika tu wako tu na pia filamu zinaandikwa kabisa kuwa hii inaangaliwa na wote na hii hairuhusiwi kuangaliwa na mtoto wa chini ya miaka kumi nane kwanini sasa watoto waangalie,” alihoji Rose Ndauka.