Wednesday , 19th Feb , 2014

Staa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania, Afande Sele, ametoa kauli nzito kuhusiana na mahusiano yake na Mama Tunda ambayo yameharibika kwa muda sasa huku asilimia kubwa ya mashabiki wakiwa katika hali ya sintofahamu kuhusiana na mustakabali wake

Katika mahojiano ambayo Afande amefanya na eNewz kwa kirefu amesema hakuja mpango wa kurudiana na mama watoto wake, na kuongeza kuwa ana furahi kuwa mwanawe Tunda kwa sasa amekuwa mkubwa ya kutosha, huku staa huyu anayependa kujulikana kama Dume la Simba akisema kuwa katika suala hili anasimamia falsafa za hayati Mzee Nelson Mandela vile ambavyo aliweza kuwasamehe watu wote waliomtendea mabaya na kushindwa kumsamehe aliyekuywa mke wake wa ndoa Winnie Mandela.

Afande Sele amesema kuwa, kutokana na Mama Tunda kumtolea heshima yake kama mume bila kufafanua zaidi juu ya hili, anaona kuwa kwa muda ambao wamekuwa pamoja imetosha na sasa kila mmoja anatafuta njia nyingine ya maisha.