Afande Sele
Itakumbukwa kuwa, heshima hii ya Ufalme wa Rhymes alipatiwa Afande Sele miaka 10 iliyopita katika mashindano ambayo hayakuwahi kuendelea tena, hivyo ameamua kufanya tukio kubwa la kuadhimisha kudumu kwa taji hilo mikononi mwake pamoja na heshima hii bila kupata mrithi ama mpinzani kwa muda wote huu.
Afande amesema kuwa, kwa sasa yupo katika hatua za maandalizi ya tukio hili kubwa ambapo atatumia muda wake mwingi jijini Dar es Salaam kuanzia sasa, ili kuhakikisha kuwa anaweka kila kitu katika mstari kwaajli ya maadhimisho haya ambayo yatafanyika mjini Morogoro.
Msikilize mwenyewe akifunguka zaidi hapa......