Monday , 29th Sep , 2014

Mtoto wa msanii wa muziki Jose Chameleone, Abba baada ya kudhihirishia mashabiki uwezo mkubwa wa kulipiga gitaa, sasa ameingia studio kurekodi kazi yake ambayo itatoka hivi karibuni.

mtoto wa msanii wa muziki wa Uganda Jose Chameleone, Abba

Abba ambaye katika umri mdogo kabisa ameonyesha kufuata nyayo za baba yake, na rekodi yake hii imepatiwa jina Game Over ikiwa tayari inangojewa kwa hamu kubwa kitaani.

Hii ni ishara na matunda mazuri ya kazi ya muziki ya Chameleone ambayo pia kwa nafasi kubwa imesaidia kuwaingiza pia ndugu zake Weasel, Palaso na AK47 katika fani hii ambayo imewafikisha mbali kimaisha.