Thursday , 26th Jul , 2018

Aslay Isihaka ameanza muziki akiwa mdogo na amefunguka kuwa katika ngoma zake ambazo amewahi fanya hadi sasa wimbo anaouheshimu ni 'Naenda kusema kwa mama'.

Msanii Aslay.

Aslay amesema hayo kwenye KIKAANGONI ya East Africa Television, inayoruka kila Jumatano kupitia ukurasa wake wa Facebook na kutoa sababu za kuuheshimu wimbo huo kuwa, ndiyo wa kwanza mara baada ya kusainiwa kama msanii.

Katika ngoma zangu, wimbo ninaouheshimu ni 'Naenda kusema kwa mama' maana ndiyo kwanza nilikuwa nimesainiwa kama msanii chini ya Mkubwa na Wanawe, hivyo wimbo huo ndio umenipa heshima hadi leo maana ulifanya nipokelewe vizuri na mashabiki wa muziki nchini”, amesema Aslay.

Msanii Aslay alianza kufahamika mwaka 2011 baada ya kutoa wimbo wake wa kwanza wa ‘Naenda kusema kwa mama’ na baadaye alitoa nyimbo nyingi peke yake kabla ya kuingia katika kundi lililokuwa na wasanii wanne likiitwa 'Yamoto Band' ambalo limevunjika na mpaka sasa anaendelea kufanya vizuri akiwa peke yake.