Friday , 29th Jan , 2016

Familia 366 zenye wakazi zaidi ya 1600 wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo na nyingine kubomoka, kufuatia mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha

Mkuu wa wilaya ya Malinyi Christina Mndeme anayeisimamia pia wilaya ya Ulanga.

katika maeneo hayo

Mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali imesababisha familia hizo kukosa mahali pa kuishi, huku wengi wao wakipatiwa hifadhi kwenye majengo ya umma ikiwemo mashuleni, kwa majirani zao au kutumi vibanda visivyo rasmi kujisitiri.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi Said Msomoka na mbunge wa jimbo la Malinyi Dkt. Haji Mponda, wameongozana kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na maafa hayo kushuhudia uharibifu huo na kutoa pole kwa walioathirika.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Malinyi Christina Mndeme anayeisimamia pia wilaya ya Ulanga amesema serikali inaendelea na tathmini kujua athari zilizosababishwa na mvua hiyo ya upepo na kuangalia namna watakavyoweza kusaidia kupitia kamati ya maafa na kusisitiza wananchi kutolima au kujenga kando kando ya mito kuepusha hasara zaidi.