
Waziri wa kazi na ajira nchini Tanzania Bi. Gaudensia Kabaka
Kutolewa kwa tamko hilo kunatokana na wakala hao kushindwa kutimiza maagizo yaliyotolewa na wizara hiyo Januari 27 mwaka huu, yaliyowataka kuwahamisha wafanyakazi husika kwa kampuni zilizokodishwa na kuwasilisha upya maombi ya usajili na uwakala kwa Kamishna wa Kazi wizarani hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika wizara hiyo, Ridhiwan Wema, ambaye amemuwakilisha Kamishna wa Kazi Saul Kinemela amesema, hadi kufikia Februari 28 mwaka huu, jumla ya maombi 56 yaliwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi, lakini ziligundulika kutokidhi vigezo na hivyo kutakiwa kukamilisha taarifa zote zinazotakiwa, vinginevyo watasitishiwa utoaji huduma.