
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini Tanzania Bi. Jenister Mhagama
Akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua vitabu vya uchambuzi wa matokeo ya kuhitimu elimu ya sekondari 2013, Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Jenister Mhagama amesema hatua hiyo itawapa morali walimu ya kufanya kazi katika mazingira ya aina zote.
Mhe. Muhagama amesema serikali inaendelea kufanya juhudi kuboresha mazingira ya ufundishaji ili kuendelea kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuajiri walimu wapya, ambapo mwaka huu serikali imeajiri jumla ya walimu 18,093 wa shule za sekondari wakiwemo 5,416 wenye elimu ya Stashahada na 12,677 wenye Shahada.