Thursday , 29th May , 2014

Baadhi ya wabunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameitupia lawama Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kitendo chake cha kuamua kuwanyang'anya ardhi wananchi kabla ya miradi husika haijakamilika.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi nchini Tanzania, Profesa Anna Tibaijuka.

Wakichangia makadirio ya bajeti ya wizara hiyo katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma, wabunge hao wamesema wizara ya Ardhi imekuwa ikifanya maamuzi ya kuwaondosha wananchi katika maeneo kwa melengo ya kupisha miradi huku miradi hiyo ikiwa haipatiwi fedha au kukamilika kwa ajili ya kuanza ujenzi wake.

Aidha, wabunge hao pia wametaka kuwepo kwa mipango miji inayotekelezeka na wametolea mfano wa jiji la Dar es Salaam ambalo kwa sasa kumekuwepo kwa ujenzi holela unaosababisha hata maeneo mengine kushindwa kupitika.

Tags: