Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya, amesema utaratibu unaotambulika kwa sasa ni mfumo wa kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita na hatimaye chuo kikuu.
Amesema mfumo mwingine ni ule wa kuanzia kidato cha nne, cheti, stashahada na baadaye mwanafunzi kujiunga na masomo ya chuo kikuu kwa vyuo pekee vinavyotambulika na baraza la taifa la elimu ya ufindi (NACTE).
Na kuhusu hatma ya waajiriwa waliotumia mfumo wa kozi mbalimbali hadi kufikia elimu ya chuo kikuu, Naibu Waziri Manyanya amesema uhakiki wa vyeti vyao utafanywa na ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora.





