Wednesday , 16th Nov , 2016

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla ameongoza kikosi kazi katika msako wa viwanda vinavyotengeneza 'pombe kali' feki ikiwemo viroba na kufanikiwa kukamata kiwanda feki kilicho maeneo ya Sinza, DSM

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wa kwanza kulia akiwa ameshika beseni lililojaa vizibo vya konyagi .

 

Akiwa katika msako huo Dkt. Kigwangalla alisema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wamefanikiwa kukamata kiwanda feki kinachotengeneza pombe aina ya viroba, konyagi, Smirnoff na zedi kilichopo sinza jijini Dar es salaam.

Dkt. Kigwangalla alisema katika msako huo wamefanikiwa kukamata kiwanda hicho kikiwa na nyenzo za kutengenezea pombe haramu kama vile chupa za konyagi, vifuniko, lebo, vifuko na nyenzo zingine za kutengenezea pombe hiyo haramu.

Alisema kuwa licha ya wamiliki wa viwanda hivyo kuwajiri vijana wengi pamoja katika kukabiliana na tatizo la ajira utengenezaji haramu wa pombe hizo kali na hatari kwa afya ya watanzania hususani vijana hivyo kufanya nguvu ya taifa kupotea.

Msako huo pia ulifanikiwa kukamata maduka yanayouza pombe hizo maeneo ya Mwenge na Manzese jijini Dar es Salaam na kuamuru wauzaji wa maduka hayo wafunge maduka yao na kuchukuliwa sheria stahiki ikiwemo kulipa faini au kufutiwa leseni za biashara.