
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania imesema inaendelea kuimarisha Huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotakiwa kupimwa vipimo vya mishipa ya fahamu pamoja na saratani kwa kutumia mashine za X-Ray na Ultra Sound katika hospitali za Rufaa za Kanda nchini.
Hayo yamebainishwa leo na wizara hiyo katika mkutano wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu kutoka katika Hospitali mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi ambapo mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Bakari Kambi, amesema serikali inafanya jitihada za kuhakikisha Hoaspitali za kanda nchini zinakuwa na mashine hizo muhimu ili kufanya kazi wakati wote ili kuwahudumia wananchi licha ya zingine kuharibika.
Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) kinawakutanisha madaktari Bingwa waliobobea katika mishipa ya fahamu inayojulikana kama wataalam wa Idiolojia kutoa mikoa mbalimbali nchini kuangazia changamoto zinazojitokeza nchini na kuathiri upimaji wa wagonjwa wanaohitaji vipimo vya X-ray.