
Katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji, mhandisi Bashir Mrindoko.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bashir Mrindoko amesema wakazi wengi wa mikoa ya Arusha, Mara, Manyara na Shinyanga wameathirika kwa kiasi kikubwa na madini hayo kwa kuharibika meno, watoto kuzaliwa na matege pamoja na wengine kuwa na vichwa vikubwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma bora ya Maji wa Wizara hiyo, Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema kiwango cha madini ya Floride ni kikubwa kupita kiasi ukilinganisha na kiwango kilichopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Wakati huohuo, waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaiujka amezitaka halmashauri za miji na wilaya nchini kulipatia shirika la nyumba la taifa NHC ardhi kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya gharama nafuu.
Akizungumza wakati wa ziara yake kwa mashirika na taasisi zinazotekeleza masuala ya ujenzi na ardhi yanayoshiriki maonesho ya biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, waziri Tibaijuka amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa nyumba, ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na kusaidia kuipanga miji na halmashauri zionekane za kisasa.