Friday , 21st Nov , 2014

Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania inaogoza kwa ukatilia wa kijinsia na watoto huku ikibainika kuwa watoto ndio wamekuwa wahanga wa kubwa katika jamii.

Baadhi ya Wananchi wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa Kilimanjaro Bi. Grace Limo wakati wa Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.

Bi. Grace amesema watoto wengi katika wilaya hiyo wanathirika kwa kutumikishwa katika shughuli za kibiashara na kwa kuachishwa shule huku wengine wakilelea na wazazi ambao wamejikita kwenye ulevi wa Kupindukia.

Siku ya kupinga ukatilia wa kijinsia huandimishwa kila mwanzoni mwa Mwezi wa Kumi na mbili ambapo maadhimisho yake huanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba na lengo la maadhimisho hayo ni kupinga vitendo va ukatili duniani juu ya Wanawake na watoto Duniani.