Visa vya Kipindupindi bado tishio Kambi ya Wakimbizi wa Tanzania.
Hofu hiyo inafuatia tathmini iliyofanywa na jopo la wataalamu wa shirika hilo na wale wa wizara ya Afya nchini Tanzania kuhusu hali halisi mkoani Kigoma na kupendekeza hatua za dharura zichukuliwe.
WHO inasema hali inatia shaka zaidi kufuatia kuthibitishwa kwa visa vya Kipindupindu kwenye kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania ambako watu 15 wameripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa kuhara na zaidi ya elfu moja wakigua ugonjwa huo.
WHO inasema kwenye kijiji cha Kagunga nchini humo ambako idadi ya wakimbizi imeongezeka kutoka 11,382 hadi zaidi ya 90,000 tangu kuanza kwa janga hilo mwezi Aprili 2015.
Taarifa ya shirika hilo inasema kuwa makundi yaliyoko hatarini zaidi ni wanawake wajawazito, watoto, wazee na makundi yanayohitaji huduma muhimu zaidi kama vile wanaoishi na virusi vya UKIMWI