Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania, Dkt. Janeth Mghamba akiongea na Waandishi wa Habari
WHO inatoa msaada wa kiufundi na uratibu ili kudhibiti kasi ya mlipuko wa kipindupindu ambao awali ulienea zaidi mji wa kibiashara wa Dar es salaam lakini sasa unatajwa kulipuka katika mikoa mingine.
Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania, Dkt. Janeth Mghamba amesema Serikali imejipanga kimkakati katika kudhibiti mlipuko zaidi wakati huu ambapo mvua za el-nino zinatarajiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki
Dkt. Janeth ameongeza kuwa kwa sasa serikali imejipanga na wataalamu mbalimbali wa afya ili kuweza kutoa huduma za haraka pindi yanapotokea magonjwa hayo ya mlipuko hususani kipindupindu.