Thursday , 25th Aug , 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba ameagiza taasisi za fedha nchini ziweke mitambo maalum ya kisasa kwa ajili ya ulinzi na kurahisisha ufuatiliaji wa matukio ambayo yataisaidia polisi kuwakamata waalifu matukio ya uvamizi.

Mwigulu Nchemba

Waziri Nchemba ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kujua serikali imeanza kuchukua hatua gani za kiusalama baada ya kutokea mauaji ya watu na askari kwenye matukio mbalimbali, ambapo amesema ofisi yake itafuatilia agizo hilo litekelezwe kwa wakati ili kunusuru majanga zaidi yasiendelee kutokea.

Kwa upande wa ulinzi kwa wawekezaji na raia wa kigeni ambao wamewekeza nchini Waziri Mwigulu amesema usalama wa biashara zao uko salama na kuwashauri wawekezaji hao kuja kwa wingi kuwekeza na wasisite kushirikiana na jeshi hilo.