Thursday , 25th Jul , 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameutaka uongozi wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo pamoja na kuondoa vikwazo vyote, ili kuvutia wawekezaji zaidi.

Waziri Mkuu Majaliwa, ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji mkoani Ruvuma, linaloendelea kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.

"Mkoa wa Ruvuma kama ilivyo mikoa mingine, una fursa ambazo zikiendelezwa zitaleta tija na kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa, nitoe rai kwa Mkoa uendelee kutangaza fursa za uwekezaji, pia muondoe vikwazo vya uwekezaji na biashara ili kuvutia wawekezaji" amesema Waziri Mkuu

"Tunapaswa kuiga kutoka wa wenzetu, Ndiyo maana Tanzania pia tunahamasisha ujenzi wa viwanda kuanzia ngazi ya Vijiji mpaka Mikoa na hatimaye kuondoa umaskini." amesema Waziri Mkuu

Kongamano hilo lina kauli mbiu kuwa 'Ruvuma itavuma kwa uchumi wa Viwanda, wekeza sasa' imelenga kutangaza fursa za uwekezaji na biashara zilizopo mkoani humu.