Wednesday , 14th May , 2014

Wizara ya Elimu an Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania imeendelea kuwahimiza wazazi kupeleka watoto wao katika vyuo vya ufundi stadi kama sehemu ya kukuza uchumi, kuimarisha ujasiriamali na pato la taifa.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania, Bi. Jennister Mhagama.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu nchini Mhe. Jenister Mhagama wakati akijibu swali la mbunge wa Bukoba Mh. Jarson Lweikiza katika kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Mjini Dodoma, aliyetaka kufahamu juhudi za serikali katika ujenzi wa vyuo hivyo.

Kwa mujibu wa naibu waziri Mhagama, hadi sasa ni wanafunzi 24,000 tu ndio waliojiunga na vyuo hivyo ikilinganishwa na nafasi zilizopo za wanafunzi 41,472, idadi inayoonesha kuwa karibu nusu ya nafasi bado hazijajazwa.

Mhe. Mhagama amesema serikali inaendelea na mkakati wa ujenzi wa vyuo hivyo katika wilaya mbalimbali nchini ili kukabiliana na wimbi la wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo hivyo.