Sunday , 25th May , 2014

Viongozi wa dini nchini Tanzania wametakiwa kuwapa elimu waumini wao namna ya kupata huduma za afya kutoka katika mfuko wa taifa wa bima ya afya kwa lengo la wananchi wenye kipato cha chini waweze kupata huduma hiyo pale wanapougua.

Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum.

Shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Musa Salum ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati viongozi wa dini ya kiislam kutoka jijini Dar es salaam waliposhiriki katika mafunzo ya namna mfuko wa bima ya afya unavyoweza kumsaidia mwananchi wa kawaida pale anapougua na kukosa huduma ya tiba kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha.

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa shirika la taifa la bima ya afya Bw. Hamisi Mdee na mwenyekiti wa bodi wa shirika Balozi Alli Mchumo wamesema huo ni utaratibu wa kawaida kwa shirika hilo kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kuwapa elimu ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na kuwasaidia wananchi.