Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Matukio yanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa hao ni pamoja na lile lililotokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasit, mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Bar ya Arusha Night Park , Mgahawa wa Vama na umwangiaji wa tindikali kwa baadhi ya watu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Arusha Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Liberatus Sabas amesema katika tukio la ulipuaji bomu Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti lilitokea Mei 5 mwaka 2013 ambapo watu zaidi ya 16 walijeruhiwa na watatu kufariki dunia,
Kamanda Sabas amesema tukio la kurushwa bomu nyumbani kwa sheikh sudi aly sudi lilitokea Julai 3 mwaka huu na watuhumiwa wengine kumi watafikishwa mahakamani kwa tukio la kupatikana na mabomu saba nyumbani Julai 21 mwaka huu, huku watuhumiwa watatu, watafikishwa mahakamani kwa kuhamasisha vitendo vya kigaidi kupitia mtandao wa kijamii