Friday , 21st Nov , 2014

Watu wanne wanao sadikiwa kuwa wezi wa ng’ombe wameuawa na watu zaidi ya 70 wenye hasira, kwa kupigwa na kuchomwa moto katika kijiji cha sheluhi wilayani Iramba, baada ya kukutwa wakiwa wamewachinja ngo’mbe hao.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Iramba ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Bwana Yahaya Nawanda amewataka wananchi wanapo wakamata wahalifu kuacha vitendo vya kujichukulia hatua za kuwauwa kwa kufanya hivyo wanakuwa hawalisaidii jeshi la polisi.

kwa upande wake mama wa mmoja wa marehemu pamoja na mashuhuda wamesema kitendo cha mauaji yaliyofanywa na wananchi wenye hasira, hawa kufanya jambo la busara kwani wange pelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Vitendo vya wananchi kuamua kuwauwa wahalifu katika wilaya ya Iramba vimekuwa vikishamiri, jambo ambalo siyo sahihi kwani wamekuwa wakipoteza ushahidi na kupatikana kwa wahalifu wengine.