Thursday , 9th Jul , 2015

Watoto watano wa familia moja wamefariki dunia na mama yao mzazi kujeruhiwa, baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto katika kitongoji cha Muleba kijiji cha Muleba kata ya Rwabwere wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Henry Mwaibambe.

Tukio hilo lilitokea Julai 6 mwaka huu ambapo chanzo chake ni kibatari kilichokuwa kimewashwa kuanguka na moto kushika nyumba hiyo ambayo ilikuwa imejengwa kwa makuti ya migomba.

Watoto waliopoteza maisha ni Zaituni Mohamed mwaka mmoja na miezi 3, Atwaibu Mohamed (4) Sajira Mohamed (3) na Shine Mohamed (7), ambao walifariki papo hapo na Khadija Mohamed (5) alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Nyakahanga

Katika tukio hilo mama mzazi wa watoto hao Sania Mohamed akizungumza katika hospitali ya wilaya Nyakahanga ameleza amepatwa na ajali hiyo wakati akiwa katika harakati za kuwaokoa watoto wake lakini hakufanikiwa kutokana na moto kumzidi nguvu.