Friday , 29th Apr , 2016

Watendaji wa Serikali wametakiwa kuwajibika kwa kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kiuchumi pamoja na kuwapatia fursa sawa za ajira kwa mujibu wa sheria.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi, na kuongeza kuwa serikali inatambua haki ya walemavu ya kufanya kazi kwa misingi sawa pamoja na kuwawezesha kiuchumi na kutoa fursa sawa za ajira.

Dkt. Possi ametoa wito kwa halmashauri zote nchini kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu ,katika fungu la asilimia 10 liliwekwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana na Wanawake kujikwamua kiuchumi.

Dkt. Possi amesema kuwa wakati Serikali inajipanga kuweka fungu maalumu kwa ajili ya kuwawezesha walemavu pekee lakini kwa wakati huu unaoendelea ni vyema walemavu hao nao wakajumuishwa kwenye asilimia hiyo kumi inayotengwa katika kwa kila halmashauri.

Naibu waziri huyo amesema fedha kuwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2010,kwa mujibu wa kifungu cha tatu na kifungu namba 34(2) lakini pia na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambavyo vinasema maana ya kubagua haitaizua serikali katika kutatua changamoto za wananchi wake.

Sauti ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi