Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto
Kamanda Muroto ametoa karipio hilo jijini Dodoma leo Jumatatu Aprili 8, 2019 ambapo ameeleza kuna taarifa wamezipata kuwa baadhi ya vyama vya upinzani watafanya maandamano kushinikiza Bunge kufuta msimamo wa kutofanya kazi na CAG Prof. Mussa Assad.
“Niwatake wale wote waliopanga kufanya maandamano kesho Aprili 9, 2019 kusitisha maandamano yao haramu, wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa,” amesema Muroto.
Mwishoni mwa juma lililopita Jumuiya za Umoja wa Vijana kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini kikiwemo ACT - Wazalendo, BAVICHA, CHAUMA, na NCCR - Mageuzi vilitangaza kufanya maandamano ya juu maamuzi ya Bunge kuhusu kutofanya kazi na CAG Assad.





