Wednesday , 16th Nov , 2016

Asilimia 80 ya watu nchini wanamiliki simu za mkononi lakini wengi wao hawana uwezo wa kuzitumia katika kufahamu masuala muhimu ya afya, elimu na kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Hassan Mshinda.

 

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Tekinolojia nchini Dk. Hassan Mshinda alipokutana na ugeni toka nchini Finland ulioongozwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo wa nchi hiyo Bw. Kai Mykkanen ugeni uliokuja nchini kwa lengo la kukagua mradi wa ushirikiano katika sekta ya Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TANZICT).

Dkt. Mshinda amesema kama serikali ikiweka mkazo zaidi katika kutumia TEHAMA kwa kuanzia ngazi ya chini ya elimu nakuweka mitahala madhubuti ambayo inatekelezeka kwa kutumia ubunifu wa fursa zilizopo basi ni wazi kwamba taifa litafanikiwa kufikia malengo yake ya milenia yaliyojiwekea.