Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Kikwete ametoa onyo hilo jana jioni Jijini Arusha, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa nne wa Mfuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50, tangu shirika hilo lilipoanza kutoa huduma mwaka 1964.
Amesema kwa sasa kumezuka tabia mbaya ya baadhi ya watu kukataa wawekezaji ambao kila nchi duniani inawahitaji ili kukuza uchumi na kuinua sekta mbalimbali hivyo ni vyema wawekezaji wakakubaliwa.
Rais Kikwete amesema ni vyema kuruhusu uwekezaji na kuondoa hofu ya kuibiwa kwa kuimarisha uboreshaji wa udhibiti wa fedha zao.
Aidha, ameitaka mifuko hiyo kupanua wigo wa kuwavutia wakulima na wachimbaji wadogo wa madini ambao ni wengi nchini kuliko sekta yoyote ili wajiunge katika mifuko hiyo, badala ya kugombania wafanyakazi
maofisini pekee.