Monday , 2nd May , 2016

Idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kifedha zinazotolewa na mabenki nchini imekuwa hairidhis

Idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za kifedha zinazotolewa na mabenki nchini imekuwa hairidhishi ambapo katika kutambua hilo Amana Benki yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeamua kutoa zawadi kwa Watanzania watakaoweka fedha zao katika benki hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo pasipo kuzichukua.

Meneja Masoko wa Benki hiyo Bw. Dassu Mussa, amesema hayo leo wakati wa kuanza kwa kampeni hiyo ambapo katika kila baada ya miezi mitatu, benki ya Amana itakuwa ikiwapatia wateja wake zawadi mbali mbali kulingana na kiasi cha akiba halisi ambayo mteja huyo amejiwekea.

Kwa upande wake, Meneja Huduma kwa Wateja wa benki hiyo Bw. Juma Msabaha, amesema kampeni hiyo itahusisha pia wateja wapya wanaojiunga nakuweka akiba zao katika benki hiyo huku ikihusisha huduma yake ya kuweka pesa kwa njia ya mtandao.