Saturday , 18th Jul , 2015

Rais mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania Alhaji Ally Hassan Mwinyi amewataka waislam na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanailinda na kuidumisha amani ya nchi iliyopo kwa maslahi ya watanzania wote.

Akizungumza mara baada ya ibada ya swala ya Eid El Fitri iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo, Rais mstaafu Mwinyi amesema wakati huu ambapo Tanzania ikiwa inaelekea kufanya uchaguzi mkuu wake hakuna budi kwa waislam na watanzania kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya viongozi wao.

Amewataka waislam na wasio waislam kuishi kwa pamoja kwa kuheshimiana na kuto farakana kwani kwa kufanya hivyo hata mwenyezi atakuwa na baraka kwa wale wote wanaoishi kwa kupendana.

Aidha Rais huyo mstaafu amewataka waislam kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu wapiga kura ili kila mtu atimize wajibu wake kwa kuwa hiyo ni haki ya kila mtu.