Saturday , 30th Dec , 2017

Mbunge wa Nzega kupitia CCM Hussein bashe, amewataka Watanzania kutokaa kimya pale wanapoona serikali inaenda kinyume, kwani wana haki na wajibu wa kufanya hivyo

Hussein Bashe ametoa ujumbe huo alipokuwa akituma salam sa mwaka mwaka mpya huku akiuaga mwaka 2017, na kusema kwamba kama Mtanzania una haki ya kutokaa kimya pale unapoona hujatendewa haki.

"Niwaombe Watanania wenzangu tusiwe wanyonge, tutimize wajibu wetu kuisaidia serikali kufanya wajibu wake, lakini tuikumbushe serikali wajibu wake, jitihada nyingi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kufanya mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya kisheria zinaweza zikawa zina maumivu, lakini zina heri mbele, lakini pale ambapo tunaona kwamba hatujatendewa haki, tusikae kimya, niwatakie kila la heri na niwaombe tujiandae kukabiliana na changamoto hizo”, amesema Hussein Bashe.

Mbunge huyo ambaye ni machachari pale anapokuwa bungeni akitetea haki za wananchi wake, ameendelea kwa kusema kwamba ...”Tuna wajibu wa kulinda nchi yetu, tuna wajibu wa kujitolea kwa nchi yetu, lakini hatuna wajibu wa kunyamazia maovu, hatuna wajibu wa kunyamazia madhambi, tuna haki na wajibu wa kupinga maovu yote ambayo tunaamini haya si yale ambayo waasisi wa taifa hilii walisimamia

Hussein Bashe amesema taifa hili lililojengwa kwa umoja na ushirikiano kuna watu walijitolea mpaka sisi tunaona ni mahali bora pa kuishi, hivyo ni wajibu wetu kulilinda.