Tuesday , 5th Jan , 2016

Watu watano na zaidi ya Ng’ombe 20, wamekufa kwa kusombwa na maji na wengine kuliwa na mamba katika mto malagarasi wilayani Uvinza mkoani Kigoma katika kipindi cha miezi sita wakati wakivusha Ng’ombe upande wa pili wa mto .

Mwenyekiti wa Wafugaji Uvinza Bw. Nyankalala Lugata

Wafugaji na wafanyabiashara wanalazimika kuvusha mifugo kwenye mto malagarasi wenye upana wa zaidi ya mita thelathini kwa kuwatumbukiza ndani ya mto huku vijana waliojiajiri kwa kuvusha wakisaidia ng’ombe kuvuka.

Akiongea na Waandishi Mwenyekiti wa Wafugaji Uvinza Bw. Nyankalala Lugata amesema utaratibu huo ambao umeanza mwaka jana baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja la kikwete umekuwa ukisabisha vifo mara kwa mara lakini kwa sasa hawana njia nyingine ya kuvusha mifugo upande wapili kwa kuwa hawaruhusiwi kupitisha juu ya daraja hali ambayo wameiomba serikali kuwasaidia kwa kujenga kivuko cha mifugo katika eneo hilo.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa wakala wa barabara Tanroad mkoa wa Kigoma mhandisi Augustine Fashe, amesema mifugo hawaruhusiwi kupita juu ya daraja hilo lenye urefu za zaidi ya kilomita mbili likiunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa kuwa watasababisha uharibifu wa barabara