Friday , 8th Apr , 2016

Serikali imeonya kuwa haitasita kumchukulia hatua afisa yoyote wa serikali atakaebainika kukwamisha vyombo vya habari nchini kutimiza wajibu wao na kuwataka waandishi wa habari kuendelea kufichua bila woga maovu na udhaifu unaotendeka serikalini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye baada ya baadhi ya waandishi wa habari kulalamikia urasimu katika utoaji wa habari unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali.

Mhe. Nnauye amesema kuwa endapo vyombo vya habari vitafichua maovu hayo serikali kali itapata nafasi ya kuweza kuchukua hatua za kutatua uozo au maovu o ya serikali huku akisema atakaebainika kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi.

Hapo awali baadhi ya Waandishi Mkoani humo walilalamikia masharti wanayopewa kutoka katika halmashauri ikiwemo ya wilaya ya Chato ambapo ukitaka kuripoti habari lazima upate kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya au Mkurugenzi.

Sauti ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akitoa onyo kwa maafisa wa serikali