Zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uras wa jamuhuri ya mungano wa tanzania kwa awamu ya tano kupitia chama cha mapinduzi limeanza rasmi mjini Dodoma kwa makada wa chama hicho waliotangaza nia ya nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa Tanzania.
Mji wa Dodoma pamoja na viunga vyake umepambwa kwa rangi za kijani na manjano za makada na wafuasi wa chama hicho ambao wamewasindikiza wagombea wanao waunga mkon.
Zoezi hilo lilioanza mapema majira ya saa nne asubuhi saa tano na saa kumi na moja jioni, kwa wagombea wa nafasi hiyo,kufika makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma, kuchukua fomu tayari kwa zoezi la kutafuta wadhamini ili kuwaunga mkono kutoka Tanzania bara visiwani.
Akiongea waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo Mh. Stephen Masatu Wasira amesema kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwa kusimamia ukuaji uchumi kwa kufufua viwanda na kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo kubwa la ajira kwa wananchi na kukomesha rushwa kubwa na ndogo,wakati wa kupata huduma mbalimbali nchini
Waliokwisha chukua fomu tayari ni Mh. Prof Mark Mwandosya, Mh. Stephen Masatu Wasira ambapo na balozi Amina Salum Ally, huku wanaotarajiwa kuchukua fomu siku ya Alhamisi wakiwa ni John Pombe Magufuri, aliyeoneonekana viwanja hivyo akimalizia hatua za mwisho, Edward Lowassa, Fredrick Sumaye, Amosi Robert Siantemi, Mohamedi Ghalib Bilali,na Balozi Ally Karume.