
Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, jaji mstaafu Joseph Warioba
Aidha Warioba amewataka wajumbe hao kujiepusha kutumia makanisa katika kutoa mitazamo waliyo nayo katika vipengele mbalimbali vya rasimu ya katiba hiyo.
Jaji Warioba ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya taasisi ya TWAWEZA ya mwenendo wa mjadala wa katiba bungeni, ambapo amesema wabunge wanatumia lugha inayoweza kuwagawa Watanzania ikiwa ni pamoja na mifano wanayoitumia katika kujenga hoja zao.