Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara , Mohammed Mpinga,
Akizungumza na East Africa radio leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabara , Mohammed Mpinga, amesema kuwa endapo wamiliki watachukua hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabari zinazosababishwa na madereva walevi.
Kamanda Mpinga amesema kuwa wameweka mkakati maalumu ambao utaanza kushughulikia kwa wamiliki wa magari binafsi na madaladala kwa kuongeza vifaa maalumu vya kupima kiasi cha ulevi kwa madereva hao.
Ameongeza kuwa kuna baadhi ya makampuni yameshaanza utaratibu huo amboa ni mzuri na unamsaidia mmiliki wa magari huku akipongeza mkakati uliofanywa na wamiliki wa mabasi ya mwendo kasi kufikiria hatua ya kuwapima madereva wao kiasi hicho cha Ulevi.
Aidha ameongeza kuwa Changamoto nyingine ni kuwapima madereva wa bodaboda ambao kwa kiasi kikubwa wamebainika kutumia vilevi wanapokuwa kazi hali inayopeleka ajali nyingine ambazo zinaweza kuepukika.