Tuesday , 10th May , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameitaka mifuko ya hifadhi za Jamii,na wawekezaji mbalimbali nchini kutoa fursa za ajira kwa wazawa ili kukuza maendeleo ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Majengo ya Mifuko Hifadhi ya Jamii nchini ya PPF na NSSF, jana Jijini Arusha Rais Dkt Magufuli amesema serikali yake inatarajia kuuona miradi mingi ya maendeleo nchini inaajiri zaidi kwa Watanzania ili kulinufaisha taifa.

Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa katika nchi zilizoendelea katika miradi mingi ya maendeleo wanafanya wakandarasi wazawa akitolea mfano wa Japan huku akiongeza kuwa ni aibu kuacha watoto wako wanakufa njaa na kuwaneemesha wa jirani.

Rais Dkt. Magufuli ameitaka Mifuko hiyo ya Hifadhi ya Jamii ikitaka kuanzisha miradi yake mbalimbali wawape kipaumbele wakandarasi wa ndani huku akibainisha kuwa lazima mifumo ya utoaji wa ajira katika miradi mbalimbali ibadilishwe.

Sauti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,akiongelea wazawa kupewa nafasi