Meneja Miradi na Biashara wa DSE Bw. Patrick Mususa
Sambamba na hilo, mauzo katika Soko hilo yameshuka kwa wastani wa asilimia 59 kutoka shilingi bilioni 6.84 hadi shilingi bilioni 2.8 kwa mujibu wa taarifa za mwenendo wa biashara katika soko kwa kipindi cha juma moja lililopita.
Meneja Miradi na Biashara wa soko hilo Bw. Patrick Mususa, amesema hayo leo na kwamba katika kipindi hicho, mtaji wa makampuni ya ndani umeongezeka kwa asilimia moja huku ukubwa wa mtaji wa soko ukibakia ule ule wa shilingi trilioni 22.
Kwa mujibu wa Mususa, kiashiria cha sekta ya viwanda wiki hii kimepungua kwa pointi 2.72 huku kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na kifedha kikishuka kwa pointi 10.36 wakati kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara nacho kikishuka kwa pointi 16.75.
Katika hatua nyingine, Bw. Mususa amesema wanafunzi 3160 kutoka vyuo mbali mbali nchini wanaendelea na ununuzi na uuzaji wa hisa na bondi katika soko hilo kupitia shindano linalolenga kuongeza uelewa wa uwekezaji katika masoko ya mitaji na dhamana.